In classrooms across Tanzania, stories are being rewritten, and futures are being shaped. Explore narratives that showcase how HakiElimu is transforming education in its 127 program schools across 22 districts in 26 regions.

Stephen Noel: A Catalyst for Change in the Heart of Mpwapwa’s Education

Stephen Noel: A Catalyst for Change in the Heart of Mpwapwa’s Education

Stephen Lwitiko Noel ni rafikiwa Elimu Katika wilaya ya Mpwapwa mkoa wa Dodoma,ambae alijiunga Katika harakati za Marafiki  elimu miaka  17 iliyopita  Katika maeneo ya Bunge kwenye maonyesho ASASI ZA KIRAIA  Katika VIWANJA vya Bunge mwaka 2007.

Mwanaharakati huyu anasema tangu ajiunge na harakati za Marafiki Elimu Katika wilaya ya Mpwapwa Kwa kushirikiana Marafiki wwnzie waneweza kuleta mabadiliko kadha wa kadha Katika Jamii ya Mpwapwa na shule nne za mradi wanazofanya nazo kazi ambazo ni shule ya Msingi Idilo,Magungu,shule ya sekondari pwaga na VIGH'AWE.

Anasema miongoni mwa mafanikio anayojivunia Katika harakati za Marafiki Elimu nikuweza kuhamasisha Jamii, juu kuchukua hatua dhidi ya changamoto zozote zinazokwamishacujifunzaji na ufundishaji, kama ubovu MIUNDO Mbinu,ukatili wa kijinsia,na uwajibikaji wa jamii Katika masuala ya kielimu.

Aidha anasema Katika shule ya Msingi Idilo waliweza kufanikiwa kushawishi Jamii kuchukua hatua dhidi ya ujenzi wa darasa la awali ambapo awali watoto walikuwa wanasoma chini ya mti, baada ya uhamasishaji waliweza kujenga darasa zuri la mfanoKwa kusaidiwa na shirika la HakiElimu.

Anaeleza kuwa sambamba na mradi wa darasa Elimu awali Sasa Jamii inatambua Umuhimu wa masuala ya mazingira rafiki ya kujifunzia na kufundishia lakini pia Jamii ya watu wa idilo na Pwaga juu utoaji taarifa za matukio ya Vitendo vya ukatili Kwa watoto majumbani na shuleni.

Pia anasema pamoja na matokeo hayo Katika Kijiji cha Magungu kata Magungu waliweza kuhamasisha Jamii juu ujenzi wa matundu Kumi na Moja ya vyoo ambapo vilijengwa Kwa kushirikiana na shirika la HakiElimu.

Hata hivyo alipoukizwa juu harakati zake zilivyo mnufaisha binafsi alusema hajuti kuongia Katika harakati hizo Kwa maana zimemsaidia kujuana na watuwengi na ameongeza mtandao wa Marafiki ambao hapo awali haikuwa hivyo," ki ukweli mimi sijuti kuingia Katika harakati hizi asee zimenisaidia sana kukurana na watu ambao zisingekuwa harakati nisingeweza kukurana nao hata Kwa dawa"alieleza.

Alisema pia harakati hizo zimemsaidia kumjengea uwezo kwe masuala mbalimbali ya uchechemuzi Kwa Jamii na anaona hatua zikichukuliwa.

Stephen Noel Kwa Sasa ambae ni CIV yaani mtoaji taarifa wa kujitolea za masuala ya Elimu na ukatili Katika wilaya yake (Community Information volunteer Kwa shule za idilo na VIGH'AWE.)