Harakati za Marafiki wa Elimu
Mpaka sasa mtandao wa Marafiki wa Elimu una wanachama zaidi ya 45,000
Marafiki wa Elimu wanafanya nini?
Marafiki wa Elimu wanashiriki kikamilifu kuchangia mawazo katika mikutano ya wazazi shuleni, kuanzisha mijadala ndani ya jamii na taifa kwa ujumla yenye lengo la kuboresha Elimu nchini, kuihabarisha jamii juu ya umuhimu wa elimu na kushawishi ushiriki wao katika michakato ya kuleta mabadiliko. Marafiki wanaelimisha jamii juu ya umuhimu wa kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa watoto mashuleni, nyumbani na kwenye jamii na kuwasiliana na viongozi wa Serikali waliopo kwenye maeneo yao mfano viongozi wa mtaa/kitongoji/kijiji/kata/wilaya na kuwasilisha matukio ya ukatili kwenye Dawati la Jinsia linapopatikana katika vituo vya Polisi nchini kwa ajili ya kushughulikia makosa yanayohusu ukatili wa kijinsia na watoto. Pia Marafiki wanaelimisha wananchi juu ya kulinda na kutetea haki ya mtoto, wanahamasisha uandikishaji na ufuatiliaji wa maendeleo ya shule, kufuatilia mahudhurio ya watoto shule hususani ufaulu katika mitihani, uwepo na utendaji wa walimu, hali ya miundombinu ya shule yaani madarasa, nyumba za walimu, vyoo na kadhalika.
Kusoma zaidi kuhusu kazi za Marafiki wa Elimu bofya hapa
Usajili wa Rafiki/Marafiki wa Elimu
Jiunge na Harakati za Marafiki wa Elimu
Ukiwa Rafiki wa Elimu utawezeshwa kupata taarifa mbalimbali za Elimu. Utapata fursa kuungana na wanaharakati wa Elimu, kutoa maoni na tashwishi kwa viongozi mahususi wa Elimu. Pia, utapata fursa kubadilishana mawazo, matarajio, na uzoefu pamoja na kujifunza kutoka kwa watu wenye mlengo wa Elimu, hivyo kwa pamoja kuchochea haki ya kila mtoto kupata Elimu bora.
Tafadhali jaza taarifa zako kwenye fomu hapo chini kwa ajili ya kujiunga na harakati za Marafiki wa Elimu.
Jiunge SasaUhakiki wa Rafiki/Marafiki wa Elimu
Hakiki usajili wako wa Marafiki wa Elimu
Ukiwa Rafiki wa Elimu uliyekwisha jisajiri unatakiwa kuhakiki taarifa zako mara kwa mara hususani anwani na maelezo mengine muhimu hasa pale unapobadili makazi, kazi. n.k
Tafadhali hakiki taarifa zako kwa kujaza fomu hapo chini.
Hakiki UsajiliOur Coverage
We are spread across 26 regions, through media advocacy campaigns and Friends of Education Network, working directly with 127 schools (65 primary and 62 secondary schools) across 22 districts:
Muleba, Serengeti, Kigoma, Geita, Kilosa, Bariadi, Ukerewe, Tunduru, Masasi, Kilwa, Mkuranga, Moshi DC, Korogwe DC, Arusha DC, Njombe, Mbeya, Sumbawanga DC, Tabora, Mpwapwa, Iramba, Musoma and Babati.
Covered Coverage Opportunity