HakiElimu inashirikiana na Taasisi ya Benjamin Mkapa, taasisi iliyopewa dhamana na Tume ya Taifa ya Mipango kuongoza uchambuzi wa kina (Deep Dive Sessions) katika Nguzo ya Uwezo wa Watu na Maendeleo ya Jamii, ambayo inajumuisha afya, elimu na uhifadhi wa jamii.
Kupitia ushirikiano huu, HakiElimu inaongoza uchambuzi katika eneo la Elimu, likihusisha sekta mbalimbali kama vile elimu ya awali, msingi, sekondari, amali na ufundi, watu wazima, elimu ya ualimu, elimu ya juu, elimu jumuishi, na mfumo wa uongozi na utawala. Lengo la uchambuzi huu ni kutathmini hali ya sasa ya elimu nchini, kuweka vipaumbele vya maendeleo, kubaini fursa za uwekezaji, na kupendekeza maboresho yatakayoleta mageuzi katika elimu kuelekea Dira ya Taifa ya 2050.
Uchambuzi huu pia unalenga kuandaa Mantiki ya Mabadiliko (Log Frame) au Nadharia ya Mabadiliko (Theory of Change) itakayosaidia kuongoza utekelezaji wa mabadiliko haya kwa mafanikio