This website is still under major improvement hence, some of the content might not be available
Marafiki wa Elimu wanafanya nini?
Marafiki wa Elimu wanashiriki kikamilifu kuchangia mawazo katika mikutano ya wazazi shuleni, kuanzisha mijadala ndani ya jamii na taifa kwa ujumla yenye lengo la kuboresha Elimu nchini, kuihabarisha jamii juu ya umuhimu wa elimu na kushawishi ushiriki wao katika michakato ya kuleta mabadiliko. Marafiki wanaelimisha jamii juu ya umuhimu wa kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa watoto mashuleni, nyumbani na kwenye jamii na kuwasiliana na viongozi wa Serikali waliopo kwenye maeneo yao mfano viongozi wa mtaa/kitongoji/kijiji/kata/wilaya na kuwasilisha matukio ya ukatili kwenye Dawati la Jinsia linapopatikana katika vituo vya Polisi nchini kwa ajili ya kushughulikia makosa yanayohusu ukatili wa kijinsia na watoto. Pia Marafiki wanaelimisha wananchi juu ya kulinda na kutetea haki ya mtoto, wanahamasisha uandikishaji na ufuatiliaji wa maendeleo ya shule, kufuatilia mahudhurio ya watoto shule hususani ufaulu katika mitihani, uwepo na utendaji wa walimu, hali ya miundombinu ya shule yaani madarasa, nyumba za walimu, vyoo na kadhalika.
Kusoma zaidi kuhusu kazi za Marafiki wa Elimu bofya hapa
![Image](https://hakielimu.or.tz//images/2024/04/22/frndppoblackb.png)