Pata habari zinazohusu elimu, taarifa zetu kwa vyombo vya habari na taarifa  za mabadiliko katika jamii ili uweze kufahamu kinachoendelea katika sekta ya elimu nchini na katika Asasi ya HakiElimu

Wafanyakazi wa HakiElimu wapewa mbinu za uandishi makini

Wafanyakazi wa HakiElimu wapewa mbinu za uandishi makini
Topics: new

Unapoandika sentensi moja kwa lugha ya kiingereza tumia maneno yasiyozidi 25. Dondoo hii imetolewa na Mdhibiti wa ubora wa kazi za Asasi ya kiraia ya HakiElimu ndugu Robert Mihayo wakati akitoa mada kwa wafanyakazi wa Asasi hiyo kuhusu makossa yanayojitokeza mara kwa mara katika uandishi wa nyaraka mbalimbali.

Ndugu Mihayo amesema unapoandika sentensi ndefu unamfanya msomaji wako ashindwe kuelewa lengo la ujumbe wako.

Ndugu Mihayo ameongeza kuwa unapoandika sentensi ni vema kuacha kuzunguka zunguka na kusoma zaidi ya mara moja ulichoandika kabla hakijaenda kwa msomaji.


Print   Email