Unashirikije Kuleta Maendeleo Kijijini?

Unashirikije Kuleta Maendeleo Kijijini?

Ushirikishaji Jamii ni jambo muhimu sana katika kufanikisha shughuli za maendeleo. Ushiriki na ushirikishaji jamii unapaswa kuwa katika hatua zote za maendeleo ya mradi, yaani kuanzia kwenye kubuni mradi, kupanga gharama na shughuli nzima ya utekelezaji wa mradi ikiwa ni pamoja na ufuatiliaji na tathimini ya mradi huo. Miradi mingi ikiwemo ya elimu haifanikiwi kwa sababu tu ya kuwatenga na kutowashirikisha wananchi katika mchakato mzima wa maamuzi ya uanzishaji, utekelezaji, ufuatiliaji na tathmini ya miradi husika. Lengo la kitabu hiki ni kufikisha ujumbe kwa makundi mbalimbali ya kijamii, wakiwemo viongozi kuhusu umu-himu wa kuwashirikisha wananchi katika michakato muhimu ya maamuzi kwa ajili ya maendeleo ya jamii. Kwa upande mwingine, kitabu hiki kinalenga pia kuwakumbusha wananchi juu ya umuhimu wao kujihusisha na mambo ya msingi ambayo serikali au viongozi wao wanawaletea, iwe mitaani au vijijini mwao. Kwa bahati mbaya wengi wao hawashiriki kikamilifu hata pale fursa zinapopatikana kwa kusingizia kuwa na majukumu mengine hivyo kushindwa kushiriki katika miradi ya jamii ikiwemo ya shule. Aghalabu hushindwa hata ku-washinikiza viongozi wao kuwashirikisha au kutekeleza miradi yao kwa mujibu wa mipango mikakati. Matokeo yake ni kudumaa kwa miradi hiyo na maendeleo kwa jumla.

File Name: CEA Publication Email.pdf
File Size: 1.29 MB
File Type: application/pdf
Hits: 865 Hits
Created Date: 02-06-2020
Last Updated Date: 02-06-2020

Related documents

Teachers Motivation Research
Teachers Motivation Research

According to the Tanzania Development Vision 2025, education plays a crucial role in bringing about social and economic transformation. In spite of its importance in bringing social and economic development, Tanzania’s education sector faces a number of challenges such as poor teaching and learning environment as well as poor learning outcomes. Poor learning outcomes can be observed in the trend of National examination results whereby in the past five years, pass rates for secondary level dropped from 89 percent in 2005 to 43 percent in 2012 and from 71 percent in 2006 to 31percent in 2012 for primary level students (NECTA,2005-2012). In addition, findings from the Early Grade Reading Assessment (EGRA) and Early Grade Maths Assessment (EGMA) show that in numeracy, less than a third of standard three students were able to do simple multiplications which they were required to learn in standard two. In English language only 6 percent of the students had basic level of comprehension in English at standard 2 levels (USAID, 2014). A national assessment called UWEZO of 2015, also shows that five out of ten pupils of standard three could not read a paragraph of standard two in Swahili. Eight out of ten of standard three pupils could not read a story of standard two in English and seven out of ten of standard three could not do a Mathematics test for standard two.

Hali ya Kisheria na Kisera kuhusu upatikaji habari
Hali ya Kisheria na Kisera kuhusu upatikaji habari

Ripoti hii ni uchambuzi na sera za Tanzania ambazo zinahitaji kufanyiwa marekebisho ili kuboresha utekelezaji wa madai ya kisheria ya kazi ya kupata habari za umma.Kupitia maswala yatafika serikalini kwa wadau muhimu na umma kwa ujumla kwa ajili ya kufanyiwa majadiliano na vitendo vinavyohitajika.