Elimu Bila malipo Utekelezaji 2017

File Name: RESEARCH_Shukia 1.pdf
File Size: 1.57 MB
File Type: application/pdf
Hits: 54 Hits
Created Date: 02-06-2020
Last Updated Date: 02-06-2020

Related documents

Je Walimu Wetu Wana Sifa na Hamasa
Je Walimu Wetu Wana Sifa na Hamasa

Utoaji wa elimu bora ni jambo muhimu katika kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Kwa hakika, waandishi wengi wanaona kuwa elimu bora ndiyo njia yenye ufanisi zaidi katika kujenga maadili, mitazamo, tabia na maarifa muhimu kwa watu binafsi ili waweze kutumika kwa manufaa katika jamii iliyotangamana. Kikao cha tatu cha Mkutano Mkuu wa 61 wa Umoja wa Mataifa (GA/SHC/3847) kilisisitiza umuhimu wa elimu bora katika kuleta maendeleo ya jamii, kikitaja kwamba elimu bora ni jambo muhimu sana katika kuleta demokrasia ya kweli na ajira ya kweli. Hali kadhalika, Dira ya Maendeleo ya Taifa (2025) inataja kwamba elimu bora ni muhimu ikiwa taifa litakubali kikamilifu kupambana na changamoto za maendeleo zinazolikabili.

Ahadi za Serikali Kuhusu Elimu 2016/17
Ahadi za Serikali Kuhusu Elimu 2016/17

Pamoja na kuwa nchi yetu imepita katika awamu 5 za utawala wa kisiasa bado changamoto katika sekta ya elimu ni nyingi. Hali ya watoto kutojua kusoma na kuandika nchini,matokeo yasiyoridhisha katika mitihani ya darasa la saba na kidato cha nne na walimu kukosa hamasa ya ufundishaji, ni baadhiya ishara za kutokuwa na mazingira bora ya utoaji wa elimu nchini na kutotimizwa kwa wakati kwa baadhi ya ahadi za serikali katika elimu. Ripoti ya UWEZO, 2015, inaonesha kuwa baadhi ya watoto wa darasa la saba hawawezi kufanya majaribio ya darasa la Pili na wanafunzi wanne kati ya kumi (44%) hawawezi kusoma hadithi ya Kiingereza ya kiwango cha darasa la pili.

Unashirikije Kuleta Maendeleo Kijijini?
Unashirikije Kuleta Maendeleo Kijijini?

Ushirikishaji Jamii ni jambo muhimu sana katika kufanikisha shughuli za maendeleo. Ushiriki na ushirikishaji jamii unapaswa kuwa katika hatua zote za maendeleo ya mradi, yaani kuanzia kwenye kubuni mradi, kupanga gharama na shughuli nzima ya utekelezaji wa mradi ikiwa ni pamoja na ufuatiliaji na tathimini ya mradi huo. Miradi mingi ikiwemo ya elimu haifanikiwi kwa sababu tu ya kuwatenga na kutowashirikisha wananchi katika mchakato mzima wa maamuzi ya uanzishaji, utekelezaji, ufuatiliaji na tathmini ya miradi husika. Lengo la kitabu hiki ni kufikisha ujumbe kwa makundi mbalimbali ya kijamii, wakiwemo viongozi kuhusu umu-himu wa kuwashirikisha wananchi katika michakato muhimu ya maamuzi kwa ajili ya maendeleo ya jamii. Kwa upande mwingine, kitabu hiki kinalenga pia kuwakumbusha wananchi juu ya umuhimu wao kujihusisha na mambo ya msingi ambayo serikali au viongozi wao wanawaletea, iwe mitaani au vijijini mwao. Kwa bahati mbaya wengi wao hawashiriki kikamilifu hata pale fursa zinapopatikana kwa kusingizia kuwa na majukumu mengine hivyo kushindwa kushiriki katika miradi ya jamii ikiwemo ya shule. Aghalabu hushindwa hata ku-washinikiza viongozi wao kuwashirikisha au kutekeleza miradi yao kwa mujibu wa mipango mikakati. Matokeo yake ni kudumaa kwa miradi hiyo na maendeleo kwa jumla.

Mazingira ya Maeneo Wanayoishi Walimu
Mazingira ya Maeneo Wanayoishi Walimu
Utafiti huu uliangalia nyanja mbalimbali zinazoweza kuchangia kuboresha au kudidimiza hali ya maisha na kazi ya walimu.Hii ilikuwa ni pamoja na:mzigo wa kazi ya ufundishaji,uwiano wa wanafunzi kwa mwalimu mmoja,maendeleo ya walimu kataaluma,athari za UKIMWI katika kufundisha na kujifunza,maisha ya walimu pamoja na maslahi ya walimu.